VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAHADHARISHWA KUTOWACHAGUA WAGOMBEA WANAOTOA RUSHWA

Na Jumbe Ismailly, SINGIDA

 


VIONGOZI wa vyama vya siasa Mkoani Singida wameshauriwa kutoyapitisha majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi katika vyama vyao watakaobainika kujihusisha na vitendo vya ushirikina ili waweze kupata nafasi za uongozi walizoomba katika uchaguzi mkuu ujao wa Raisi,Wabunge pamoja na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba,mwaka huu.

 

Ushauri huo umetolewa na Naibu Amiri JASUTA Mkoa wa Singida,Sheikh  Abdurahmani Hassani alipokuwa akiongea na waumini wa dini ya kiislamu kwenye viwanja vya msikiti wa AL-FORUQAN,uliopo Kata ya Minga, Manispaa ya Singida.

 

Aidha Naibu Amiri huyo hata hivyo akawasisitiza pia waumini wa dini hiyo kutowachagua wagombea wanaojihusisha na tamaa ya madaraka ya uongozi kupitia vitendo vya ushirikiana.

 


“Ikibainika mimi nasema na ninashauri ikibainika kwamba mgombea ni mshirikiana na anafanya makafara,anafanya ushirikiana asipewe kura hata moja akijulikana na akabainika na zipo alama za mshirikina,mkimuoina anafanya vitu vya ajabu,anatoka usiku anakwenda kuoga maji njiapanda

usiku”alisisitiza Naibu Amiri huyo.

 

Aidha Naibu Amiri huyo hata hivyo aliweka bayana kwamba endapo mgombea wa aina hiyo akibainika,vyama vya siasa visipitishe jina lake kuendelea na mchakato wa kugombea kwenye nafasi hiyo ya uongozi.

 

Alisema kiongozi huyo kwamba viongozi wenye dhamira nzuri ya uongozi katika maeneo ya kata,jimbo na nchi wawe ni watu wenye hofu ya mungu,wenye uchamungu na wenye imani na ambao pia siyo wapagani kwa kutomwabudu mungu na badala yake wakawa wakimwanini shetani.

 

Masozi Abdala ni Amirati katika msikiti wa Al-Shababu mjini Singida alibainisha kuwa idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakiangamia kutokana na maadili wanayopendelea kuyatekeleza kuwa yapo kinyume na maandiko ya mwenyezimungu katika maisha yao ya kila siku

 

Kwa mujibu wa Amirati huyo akina mama wengi wanaangamia kutokana na vitendo vya ushirikana na upo uwezekano mkubwa wa akina mama hao kuingia motoni kutokana na kujihusisha na vitendo vya ushirikina kwa kutojiamini kwenye ndoa zao.

 

“Mwanamke yupo radhi amuharibu mume wake lengo tu avutie kwamba mume aweze kumpenda hicho ndicho kitu kikubwa sana kwa akina mama na kuwavutia wanaume ili watupende sisi kuliko familia zao huo ni mtihani mkubwa sana”alifafanua Masozi.

 

Alibainisha Masozi kwamba licha ya kwamba idadi kubwa ya wanawake wanaipenda dunia kuliko maarisho ya mwenyezimungu,lakini wakumbuke kwamba hapa duniani ni mapito tu na hakuna mtu atakayeishi milele na mwisho wa siku watakwenda kuulizwa.

 

Ili kukabiliana na vitendo hivyo vya ushirikiana Amirati huyo alisisitiza kuwa kikibwa zaidi ni kinamama kujitahidi kuitafuta elimu ya akhera kwa kwenda kwenye madrasa ili waweze kujifunza ni nini kilichowaleta hapa duniani na kikubwa zaidi ya yote ni kufanya ibada na hakuna zaidi ya hilo.

 

Akizungumzia suala la mmomonyoko wa maadili,mmoja wa waumini wa msikiti wa Al-Forouqan,Ahmadi Daudi Masilamba alisema tangu kituo cha Markasi kilipoanzishwa zaidi ya wanafunzi 1,000 wamepatiwa masomo yao ya dini na kwamba taarifa zilizopo ni wanafunzi waliopitia katika Markasi hiyo wamekuwa wakifanya vizuri na wanaendelea kuwa masheikh wazuri kwenye misikiti waliyopo.

 

MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post