Na Amini Nyaungo
Shirika la Umeme Tanesco limeanzisha mfumo wa namba ya kupiga simu kwa namba180 ili wateja wao wapate huduma kwa haraka zaidi pindi wanapopata matatizo yanayotokana na umeme ili watatuliwe tatizo lao haraka.
Hayo ameyazungunza leo Rehema Mwaipopo Afisa Uhusiano na huduma kwa wateja TANESCO Mkoa wa Singida alipoongea na Standard Radio katika kipindi cha asubuhi na kusema kuwa kwa sasa hiyo namba ni muhimu sana pindi unapopata matatizo yanayohusiana na umeme.
"Tanesco tuna namba yetu hivi sasa piga 180 unapopata matatizo ili tukuhudumie haraka shida yako," Rehema
Katika hatua nyingie Mwaipopo ameweka bayana kuwa kutokana na nishati safi TANESCO wamesisitiza kutumia nishati safi kwa kutumia umeme huku akisema kuwa matumizi ya umeme sio gharama kama ambavyo wanasema watu wengi.
"Tuna majiko ambayo yanatumia umeme kidogo tunawashauri wananchi wapikie vyakula vyao kwa kutumia umeme, maharage yanaiva kwa chini ya uniti moja hivyo msiogope,"Rehema
Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kutunza miundombinu ya umeme ili huduma hiyo iwe katika wakati mzuri, aidha Rehema amewataka wananchi kuwa walinzi wa Transfoma zao kwani kuna wizi unafanyika ambao unarudisha nyuma maendeleo.
Aidha ametumia nafasi hiyo kusema kuwa ni hatari sana kuiba vifaa vya umeme kwani wanaweza kuangamia,"
Kwa upande wa Injinia Ernest Nyerere akizungunzia usalama wa watumiaji wa umeme amesema kuwa watu wanatakiwa kuwa na tahadhari watumie mafundi wanaotambulika pamoja na kuyafanya yote yanayohusu umeme wawaite watu wa umeme.
Pia amesema watu wasifanye shughuli yoyote chini ya miundombinu ya umeme kwani ni hatari.
"Tanesco tunawashauri wananchi wasifanye shughuli zozote za kibinadaam katika miundombinu ya umeme,'' Ernest
"Tunawatahadharisha wananchi wafanye wiring ya umeme uliokuwa bora na baada ya miaka mitano wakague.
Katika hatua nyingine Ibrahimu Solo kutoka Idara ya habari ya Tanesco Mkoa wa Singida amewahimiza wananchi kuunganisha huduma ya umeme katika nyumba zao.
Mwisho


Post a Comment