Amini Nyaungo
Jamii imetakiwa kuenzi
mila na desturi chanya zinazochangia ujenzi ambazo hulithishwa kutoka kizazi
kimoja kwenda kingine.
Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii , Jinsia na Makundi Maalum, Amon Mpanju katika uzinduzi wa kitini cha
majadiliano ya Mila desturi katika kijiji cha Ighombwe Mkoani hapa siku ya jana
Juni 2,2025.
Akisema kuwa ni muhimu
sana kwa jamii kuangalia tamaduni zilizochanya
ambazo zinafaida kwa jamii.
“Jamii inatakiwa
kuangalia mila na tamaduni zilizokuwa sahihi katika jamii ili kuziendeleza na
kulithishwa kwa jamii,” Mpanju
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Rashid Mohamed Rashid amesema kuwa kupitia majadiliano hayo
wananchi wamejua kuziacha mila potofu.
“Katika majadiliano haya
yaliyofanyika jamii imejua mila potofu na kuziacha hivyo naamini itakuwa vyema
kuziacha mara moja zile zisizokuwa sahihi,” Rashid
Aidha kwa upande wa
wananchi ambapo walikuwa wanatoa mrejesho baada ya majadikiano wamesema mila
mbaya ni pamoja na Chagulaga, Ukeketaji na kurithisha wake.
Mwisho
Post a Comment