Na Robert Onesmo
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida Jesca David Kishoa, ametoa zaidi Milioni 3 za kitanzania kwaajili ya ukarabati wa barabara inayoelekea katika ofisi ya kijiji cha Iguguno kilichopo kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Kishoa amekabidhi fedha hizo June 22 2025 baada ya kutoa ahadi hiyo wiki kadhaa zilizopita ambapo amesema ametoa fedha hizo ili kukarabati barabara hiyoo jambo ambalo litarahisisha viongozi na wananchi kufika katika Ofisi hizo bila changamoto.
Moja ya viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho amesema wanatoa shukrani za dhati kwa Mbunge Kishoa kwa kuwiwa na kufanya jambo la kiungwana la kuboresha miundo mbinu hiyo inayofika katika ofisi ya kijiji huku akiweka wazi kuwa endapo zoezi hilo la ukarabati wa barabara hizo likikamilika litakuwa limeondoa changamoto kubwa .
Mwisho



Post a Comment