Na Robert Onesmo, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego, ametangaza kuzinduliwa kwa kamati ya Ushauri wa kisheria ngazi ya Mkoa itakayo zinduliwa rasmi May 19 2025 katika viwanja vya stendi ya zamani Mansapa ya Singida
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dendego amesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa may 19 itaambatana na kliniki ya sheria bila malipo kwa wananchi wote Mkoa wa Singida
Kwa upande mwingine Dendego ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili waweza kutibiwa kisheria katika mambo ambayo yawawatatiza.
Kwa mjibu wa Matrider Meckson ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Sheria Mkoa wa Singida amesema zaidi ya wanasheria 50 watakuwepo katika kliniki hiyo hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kupata huduma hiyo bure.



Post a Comment