RC DENDEGO ATEMBELEA KABURI LA SHUJAA LITI UTALII WA NDANI SINGIDA

 



Na Sylvester Richard

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Halima Omary Dendego ametembelea Kaburi la Shujaa Liti ambaye ni Malkia wa kabila la Wanyuturu kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.


Dendego amefanya ziara hiyo Aprili 27, 2025 akiambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na zimamoto na uokoaji.

Aidha, akiwa kaburini hapo amewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Singida na wageni wanaofika Mkoani Singida kusherehekea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (MEI MOSI) kufika kwenye kaburi la Shujaa huyo Mwanamke lililopo katika Kijiji cha Makuyu Singida pamoja na maeneo mengine yakiwemo makazi ya Mtemi Senge na Ziwa Kinda maeneo ambayo yanapatikana Manispaa ya Singida.
Ametumia nafasi hiyo  kuwaelekeza wananchi kumuenzi Shujaa Liti kwa kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuchagua viongozi bora na kuahidi kujenga Chuo cha nyuki kando ya Kaburi  la Liti kwakuwa Malikia huyo alipambana na wakoloni wa Kijerumani kwa kutumia nyuki.
Shujaa Liti alizaliwa mwaka 1860 na kufariki mwaka 1907 baada ya kukatwa kichwa na wakoloni wa Kijerumani ambao waliondoka na kichwa hicho hadi sasa ambapo Mkuu wa Mkoa Mh. Dendego ameahidi kufuatilia mpaka kichwa hicho kitakaporejeshwa Nchini kama kilivyorejeshwa kichwa cha Mkwawa Shujaa.

Post a Comment

Previous Post Next Post