Na Amini Nyaungo
Vijana wametakiwa kuyaishi na kuyafanyiakazi mafunzo ya ITIFAKI yanayofanyika kwa siku mbili mkoani Singida ikiwa ni moja ya wasifu mkubwa kwa mshiriki mwisho wa mafunzo hayo.
Hayo ameyasema jana Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Singida Mjini Ndugu. Lucia Mwiru wakati akifungua mafunzo ya ITIFAKI yaliyofanyika Singida mjini akiwa mgeni rasmi aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe.
Mwiru amesema kuwa vijana wanatakiwa wajitambue na ni fursa kubwa kwao kwani mwisho wa mafunzo watatambulika na huenda ikawasaidia katikaa wasifu wao wanapoomba kazi mahali pamoja na kuelekea sherehe za Mei Mosi zitakazofanyika mkoani Singida.
"Niwaambie tu mpo sehemu salama jitahidini kuweni na nidhamu mtu wa ITIFAKI anatakiwa awe na nidhamu hii itawasaidia siku zijazo pamoja na kuelekea Mei mosi," Mwiru.
Aidha Mkuu wa ITIFAKI Wilson Silvester amewapongeza watu wa Mkoa wa Singida kwa kujitolea kwako na kushirki mafunzo hayo ya ITIFAKI huku akiwataka wasikate tamaa katika kuyatafuta maisha.
" Niwasihi maisha ni mapambano msikate tamaa huwezi juu Mungu amekupangia nini, niwapongeze kwa kuja kwa wingi katika mafunzo haya,"Wilson
Wakati huo Mkurugenzi wa ITIFAKI Kanda ya Kati Omary Hamis amewapongeza ITIFAKI taifa kwa maono yao na kuja kufanya mafunzo mkoani Singida,"Omary.
Mafunzo hayo yatarajiwa kufungwa tarehe 14,04,2025 baada ya washiriki zaidi ya mia moja na themanini (180) kushiriki mafunzo hayo.
Mwisho.






Post a Comment