Na Robert Onesmo
Mmeona ile mipira ya kutenga jana (set pieces kick )iliyopigwa na Decline Rice ,mipira ambayo yote iliingia kambani bila Thibaut Courtous kuigusa wala kuiona??
Kuna kicha mmoja wa kutoka viunga vya mji wa Belrin Ujerumani ,anaitwa Nicolas Jover, huyo mwamba unaambiwa ni moto wa kuotea mbali ,ni moja ya katika ya makocha bora wa mipira ya kutenga,...wasifu wake ni upi??
NICOLAS JOVER alizaliwa October ,28 ,1981(43) huko Berlin Ujerumani ,Nicolas hakuwahi wala hajawahi kuingia uwanjani kucheza soka la ushindani wala kufundisha mpira kama kocha ,mapema baada ya kufikisha miaka 20 Nico alianza harakati za kusomea degree ya michezo (sport Degree )katika chuo cha michezo cha Sherbrooke kilichopo Canada na baada ya kuhitimu hapo akaenda Ufaransa kujiunga na klabu ya Montpelleir mwaka 2009 -2016 akiwa kama mtaalamu wa kusoma na kuchambua matukio ya timu(Video Analysis)wakati kabla ya hapo alikuwa mchambuzi wa mechi za timu ya taifa ya Croatia hiyo ikiwa ni mwaka 2013
Na 2016 -2019 Nicolas alijiunga na Brentford kama kocha wa mipira ya kutenga (SET PIECES COACH),2019 -2021alijiunga na Manchester city na baada ya hapo Jover akajiunga na Arsenal na ndio mpishi mkuu wa mipira hiyo kama ambavyo uliona jana wakati Rice anachukua mali alinyanyuka na kumpa ishara ya kwa kuukunja mkono wake (inside Curve)au Banana kick...huku kwenye PES sisi tunaita mzungusho.
Na Huyo ndio NICOLAS JOVER je wewe unamfahamu kocha wako wa Set pieces kick?



Post a Comment