RC DENDEGO ATOA MCHONGO MZITO SINGIDA

Na Amini Nyaungo



Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewaomba wakazi wa Singida wajiandae kwa fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa kupokea wageni zaidi ya elfu sita watakao kuja mkoani hapa kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani.

Dendego ameyasema hayo jana (March 26,2025)katika Iftar iliyoandaliwa na Biostutain ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa wasilale wafanyekazi ipasavyo ili wanufaike na fursa hizo zitakazojitokeza za ugeni huo.



" Kama unaendesha bodaboda basi endesha kweli, kama unanyumba za wageni ziboreshe, kama hujasajili nyumba yako isajili ili wageni hao wapate hifadhi na uweze kujipatia kipato.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba kudumisha matendo mema waliyoyafanya ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani waendelee nayo hadi mwisho wa maisha yao.

"Amani, upendo na ustaarabu ambao tumeutengeneza ndani ya mwezi wa Ramadhani basi udumu katika maisha yetu ya kawaida baada ya mwezi wa radhani," Dendego.

Mwisho 

Post a Comment

Previous Post Next Post