KISHOA ATOA MILIONI 6, ASAIDIA WANYONGE

 Na Amini Nyaungo

Kijiji cha Nkalakala kimepata fedha milioni sita kutoka kwa Mbunge wa  Viti Maalumu Mkoa wa Singida Jesca Kishoa ambazo zitatumika katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamefanyika leo Februari 16,2025 katika kijiji cha Nkalakala Wilaya ya Mkalama ambapo Mbunge Jesca Kishoa amezitoa kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo shule, Zahanati, Michezo na walemavu.

Kishoa ametumia nafasi hiyo kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo kusaidia walemavu juu ya  usafiri na pesa za kujikimu.


Kwa upande wa wanafunzi wa kike ametoa taulo za kike kwa shule za kata ya Nkalakala.

Wananchi wamesema kuwa wamefurahishwa na namna ambavyo Jesca Kishoa anawafanyia watu wa Mkalama.


Mwananchi Sara Saidi ameshukuru na kusema kuwa mbunge huyo anaendelea kuwafanyia yaliyo mazuri katika Wilaya hiyo ya Mkalama.

"Namshukuru kwa hiki anachoendelea kutoa Jesca Kishoa kwetu sisi," Sara


Hussein Said amesema kuwa jezi ambazo amezitoa kwao zitawasaidia katika kunyanyua vipaji vyao.


"Hizi jezi zitatusaidia katika kukuza na kuendeleza vipaji vyetu,"amesema.

Aidha katika hatua nyingine Kishoa ametoa mitungi ya gesi kwa kina mama lishe, ametoa jezi za mpira pamoja na taulo za kike kwa shule za msingi na Sekondari katika eneo hilo.


Kwa upande wa Serikali amemsifia Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mikubwa ya maendeleo.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post