HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WANANCHI JITOKEZENI KUTOA TAARIFA ZA UKIUKWAJI WA MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA

Na Charles Kikoricho

Ofisi ya Rais , Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma kanda ya kati  imewaomba Wananchi kujitokeza kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma. 
Hayo yamesemwa hii leo  November 6/2024  ofisini kwake na Bi. Jasmin Awadhi Bakari, Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais,  Sekretarieti ya Maadili ya Uongozi wa Umma kanda ya kati ametaja Majukumu yao  tisa ambapo ni pamoja na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambayo yamefanywa na viongozi wa umma kwa kukiuka maadili ya viongozi kwa njia mbalimbali kama vile kuandika barua kwa sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma, kufika mwenyewe ofisini, kupigia simu na taarifa hizo  sio lazima ujitaje jina lako wala kuandika namba yako ya simu ilimradi tu utaje jina la kiongozi ambaye unamlalamikia na sehemu anayopatikana na amefanya nini, kufanya uchuguzi wa awali kujua amefanya nini, kufanya uchunguzi kutokana na taarifa mbalimbali kama vile kupitia vyombo vya habari, Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali yaani CAG, au taarifa mbalimbali kutoka kwenye ofisini za serikali za utekelezaji kwa umma , kufanya uhakiki na uchunguzi wa taarifa ambazo wamezipokea kutoka kwa viongozi wa umma, kutoa elimu kwa viongozi kuhusu maswala ya Maadili kwa viongozi


 pamoja na Wananchi kwa ujumla, kufanya utafiti kuhusu hali ya maadili kwa viongozi wa umma nchini na kutoa ushauri wa mwenendo wa hali ya maadili nchini, kuweka mikakati na kutunga mikakati ya namna ya kukabiliana na mambo mbalimbali yanayohusu maadili kwa viongozi wa umma.
Viongozi wa umma kwa mujibu wa sheria wanawajibu wa kutoa tamko la mali zake na madeni  na kwa mujibu wa sheria taarifa hizi zinatolewa kwa vipindi vitatu kwanza baada ya kiongozi kuteuliwa ndani ya siku 30 baada ya kuteuliwa na kuthibitishwa katika nafasi ya uongozi, kipindi cha pili ni kila mwaka anatakiwa kuwa anatoa tamko kila mwaka inapofika  December na mwisho wake huwa ni December 31 ,lakini pia kiongozi anapotoka kwenye ofisi ya Umma miezi mitatu au kabla ya miezi mitatu anatakiwa awe ametoa taarifa hizo.
Jasmin  amesema kuwa ofisi hiyo ni ya  wananchi wote hivyo wanayo ruhusa ya  kutoa malalamiko mbalimbali yanayohusu ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma kwa njia mbalimbali kama vile kuandika barua na kuituma kwa njia ya posta S.L.P 1887 Dodoma, kupiga simu 0262160190 ,kuandika barua pepe dodoma@maadili.go.tz, au kupitia mitandao ya kijamii Facebook, Instagram pamoja  na X kwa kuandika Sekretarieti ya Maadili lakini kwa njia ya  website www.maadili.go.tz kuna sehemu ya kuandika malalamiko na watu wote iwe ni Mwanachi wa kawaida, au kiongozi unaruhusiwa kutoa malalamiko yako ya ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma, mfano  iwe ni kumuona kiongozi anatumia madaraka yake vibaya au kujilimbikizia mali,anafanya upendeleo, anatumia vibaya mali  za umma na mambo mengine ambayo ni ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma unaruhusiwa kutoa taarifa.
"Mwananchi anaweza kutoa maoni yake kupitia barua pepe au katika mfumo wetu kama ambavyo nimetangulia kusema," Jasmin
Bi. Jasmin  amewakumbusha pia viongozi wa umma kwamba kuenaelekea katika kipindi cha kutoa matamko ya Rasimali na madeni na tayari kamishna ya tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma ameshatoa matangazo kwamba mwaka huu matamko yatatolewa kwa njia ya mfumo na mfumo unapatikana kupitia www.maadili.go.tz ukiingia pale utaona namna ya kutoa taarifa zako.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply