Na Amini Nyaungo
Shirika la Farm Radio International (FRI) jana tarehe 04.11.2024 iliwafanyia mafunzo Waandishi wa Habari ya namna ya kufanya vipindi vya Radio ikiwemo vipindi vyao vya miradi wanayoisambaza katika Radio mbalimbali hapa Tanzania.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo namna ya kufanya vipindi mbalimnali pamoja na vipindi vyao vya miradi ambavyo huwa wanawaletea Radio mbalimbali hapa Tannzaia kwa ajili ya utekelezaji, moja ya vipindi vyao kilimo ambapo kwa sasa wanaendeleza mradi wao wa miaka mitatu wa IRESAP unaohusu kilimo.
Mkurugenzi wa Farm Radio International kwa Tanzania Susuma Susuma aliwapongeza Waandishi wa habari ambao waliokuwa wanautekeleza mradi huo kwa kufanya vizuri huku akiweka bayana kuwa jitihada zao ndio zimefanya kupatikana mradi huo ambao unaoendelea.
"Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya naamini mradi huu umeendelea kuwepo kwakuwa ule mradi uliopita mlifanya vizuri, tuendelee kushirikiana na kufanyakazi kwa juhudi,"Susuma
Aidha Susuma alisema kuwa katika mikakati yao awamu ya kwanza ya mradi walikuwa na lengo la kuhimiza mbinu za kilimo Ikolojiahulu awamu ya pili ilikuwa na mambo manne, moja kukazia yale yaliyopita ya awamu ya kwanza, pili kupanua wigo wa elimu , tatukufanya uchachamuzi pamoja na kuongeza Radio zinatakazoendelea kutoa elimu ya kilimo na ufugaji.
Naye Mratibu wa Radio na Watangazaji wa Farm Radio Esther Mwangabula amesema kuwa wamekuja kwa ajili ya kuwakumbusha namna ya kufanya vipindi kama ambavyo mara zote huwa wanafanya.
Anatamani kuona Radio zinafanya vizuri na wanaendelea na ubunifu ili vipindi viwe vizuri zaidi.
"Lengo la kuja leo ni kuwakumbusha na kuboresha ufanyaji wa vipindi uwe bora, endeleeni lufanya vizuri,"Mwangabula
Mwangabula amesema awamu hii kutakuwa na vipindi vinne ambavyo mtindo wake utakuwa tofauti na vile kumi vilivyopita amesema kuwa aina ya "Script" haitakiwa kama ile na ametoa mafunzo namna ya kuvifanya hivyo vipindi.
Naye Mkuu wa TEHAMA Farm Radio International Calorine Kimario amesema kuwa katika mfumo wa kupaza sauti utakuwepo lakini kuna maswali wakati vipindi vimaendelea na ameweza kutoa mfano wake namna vipindi hivyo vitakavyo kuwa
"Katika vipengele vilivyoongeza katika paza sauti kuna swali limeongezeka wakati kipindi kikiwa hewani,"Kimario
Katika mafunzo hayo Waandishi wa habari kutoka Radio tano za kanda ya kati na Kaskazini wamenufuaika nayo ni pamoja na Standard Radio ya Mkoani Singida, Mwangaza FM ya Dodoma, Lumeni ya Karatu, Utume ya Tanga na Radio Kicheko ya Kilimanjaro.
Mwisho
No comments: