Na Amini Nyaungo
Wakati mradi huu ulipoanza kila mmoja alikuwa na maswali mengi itakuaje kipi kitafanyika je waliopitiwa na mradi huu watalipwaje.
Kwanza tuujue kwa ufupi mradi huu ambapo ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania. Mradi huu una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania. Bomba linapita katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Bomba vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.Wahusika wa mradi wamepita kwa kila kaya ambayo imepitiwa na mradi kufanya tathimini ya mali zao na baada ya kupata thamani wakawapa nafasi kuwauliza wawape hela wakajenge nyumba au wawajengee nyumba, wale waliokubali wamejengewa nyumba ambazo zina kila kitu kinachotakiwa katika nyumba.
Kama haitoshi wamewalimia mashamba kwa kutumia kilimo bora ambapo kwa ushuhuda wa waliolimiwa wanasema kuwa haijawahi kutokea wakapata gunia 30 kwa msimu mmoja hivyo imewanyanyua kiuchumi, lakini wale waliokuwa na mifugo ya kuku basi wamejengewa mabanda imara ya kisasa ya kuku, halikadhalika wale wafugaji wa Ng'ombe nao walipatiwa mbegu bora na elimu ya ufugaji bora.
Hii sio kujali bali kuwapa maisha wale waliopitiwa, nimewahi kuona miradi mingi ila huu wa bomba la mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ndio bora zaidi.
Lakini pia wahusika wamepewa chakula mwanzoni kabisa mwa mradi ulipoanza ni chakula ambacho kimethibitishwa na watathimini ubora (TBS).
Elimu hii nimeipata baada ya kupata semina ya wahusika kutoka katika mradi huu na wameweza kuonesha namna walivyopita na ushahidi wa picha mjongeo kwa wahusika waliopitiwa na mradi.
Kikubwa ambacho wamezingatia mila na tamaduni za watu, walifika sehemu makabila hawataka kuondoa makaburi ilibidi wazunguke eneo hilo pale ambapo walitaka kufanya tambiko za kimila waliweza kuchangia baadhi ya mahitaji.
Hii tunaweza kusema mgeni njoo mwenyeji apone ndio ilivyo kwa mradi huu ambao umebadilisha kabisa maisha yao na kufa ya mwanzo wao mpya wa maisha.
ILIKUAJE HADI IKATOKE MRADI HUU KUANZA ?
Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.
UNAWEZA KUJIULIZA JE LENGO LA MRADI HUU NI UPI ?
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa nchini Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Mkoa wa awali kwa Tanzania ni Kagera (Bukoba Vijijini, Muleba na Biharamulo), Geita (Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe ,Shinyanga (Kahama Mjini);Tabora (Nzega Vijijini, Nzega Mjini na Igunga);Singida (Iramba, Mkalama na Singida Mjini); Dodoma (Kondoa na Chemba);Manyara (Hanang na Kiteto) pamoja na Tanga (Kilindi, Handeni Mji, Handeni Vijijini, Korogwe, Muheza na Tanga Mjini.
Bomba la mafuta linapitia katika mikoa nane na wilaya ya 24 zaTanzania Bara kama ambavyo nimeorodhesha juu.
Tanzania hii sio mara ga kwanza kushirikiana na nchi jiranj katika maswala ya maendeleo, kwani zamani iliwahi nabado inaendelea bomba la mafuta na (TAZAMA) ambapo linahusu Tanzania na Zambia huku Reli kati ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
FAIDA ZAKE KAMA TAIFA
Licha ya kupata pesa lakini pia ni nzuri katika Diplomasia na kudumisha undugu kumbuka Tanzania ina utajiri wa bahari huku Uganda ni nchi ambayo "Land locked Country" hivyo bodjaa zake nyingi lazima zipite katika nchi ambazo zina bahari.
Urafiki utadumu sana kwa kuwaa na miradi mikubwa kama hii ambayo inaleta tija.
Ajira zitapatikana nyingi kwa wazawa ikumbukwe bomba hili limepita sehemu kubwa hapa nchini kwetu Tanzania hivyo ajira zitakuwa nje nje.
GHARAMA ZA MRADI HUU HADI KUKAMLIKA
Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili litajengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
NANI APONGEZWE ?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuitekeleza miradi mikubwa kama hii pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kusamia vizuri.
Bila kuwasahau wasaidizi wa Marais wa idara hii kwa pande zote za nchi mbili yaani Uganda na Kenya.
Mwisho.
No comments: