HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WANAHABARI SINGIDA WAIBAMIZA TIMU YA MANISPAA

Timu ya mpira wa miguu ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Singida imeshinda penati 7 kwa 6 dhidi ya timu ya Manispaa ya Singida katika tamasha la Muungano lililofanyika uwanja wa Bombadier mkoani hapa  lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego. 

NYOTA WA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SINGIDA AMINI NYAUNGO "KIRAKA" JEZI NAMBA 11 AKIUTAFUTA MPIRA KWA KASI

Dakika tisini za mchezo huo zimetoshana nguvu kwa kutokufungana ambapo muamuzi ameamuru kupigwa penati ambazo zimetosha kuwafanya wanahabari kuibuka na ushindi kwa penati 7-6.


Shukran za kipekee zimuendee goli kipa wa Waandishi wa Habari mkongwe Cales Katemana ambaye aliokoa penati moja ambayo ndio imewafanya Waandishi wa Habari kuibuka na ushindi. 

BAADA YA GOLI KIPA WA WANAHABARI SINGIDA CALES KATEMANA KUDAKA PENATI YA MWISHO WACHEZAJI WENZAKE WAKISHANGILIA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego aliahidi kununua goli moja kwa shilingi elf hamsini kwa kila timu itakayopata goli ndani ya dakika tisini na baadae kutekeleza ahadi yake kwa kutoa zawadi hizo. 



Kwa mujibu ya Waandaaji wa tamasha hilo kutokana na muda ubingwa imepewa timu ya ITIGI ambayo imefunga magoli mengi katika mechi yao ambayo wamepata magoli manne huku Tanesco wakishika nafasi ya pili.


Katemana kutoka Waandishi wa habari kaondoka na elfu ishirini kwa kunyakua penati na kipa bora wa michuano hiyo.


Katika tamasha hilo ambalo lilikuwa na michezo mbalimbali Ikiwemo kuvuta kamba, kufukuza kuku Wanawake na Wanaume, kukimbiza na magunia.


Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amesema kuwa tamasha la namna hiyo litafanyika kila mwezi mara moja. 

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply