WANANCHI WAHIMIZWA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

 

Na Sylvester Richard.



Wananchi wa Mkoa wa Singida wamehimizwa kuwalinda watoto ili wafikie utu uzima wakiwa na afya njema. 


Rai hiyo imetolewa Juni 25, 2026 na Sajenti wa Jeshi la Polisi Ernest Orondo kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida kitengo cha dawati la jinsia na watoto alipokuwa akitoa elimu ya madhara ya ukatili dhidi ya watoto kupitia Radio Standard Singida . 



Sajenti Orondo amesema ni vizuri kuwekeza kwa watoto kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi na malezi yenye maadili mema jambo ambalo litatengeneza jamii bora yenye kujiamini katika kuleta maendeleo yao na taifa kwa ujumla.  



Toka dawati la habari Singida.

Post a Comment

Previous Post Next Post