Na Amini Nyaungo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari amewataka wananchi kuwa na imani na taasisi zinazotoa haki huku akisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kuboresha huduma hizo.
Hayo ameyasema leo April 22,2026 katika hafla ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu iliyofanyika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wakikabidhi magari ya shirika lisilo la Kiserikali la SEMA.
Baada makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Shirikia lisilo la kiserikali la SEMA Ivo Manyako mkoani Singida ameishukuru serikali kwa kurejeshewa magari yao ambayo yalichukuliwa ambapo magari hayo yatasaidia kuendesha shughuli zao za kila siku. Hayo ameyasema leo April 22,2026 Mkoani Singida wakati wa hafla na mwanasheria Mkuu wa Serikali iliypfanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida.
Magali hayo yalichukuliwa na dalali wa Mahakama baada ya kesi iliyohusu kuungua kwa magari yaliyokuwa ndani ya Karakana ya shirika hilo.
Mwisho




Post a Comment