Na Amini Nyaungo
Wananchi wametakiwa kuwa na usafi wa mazingira ili kuepuka kuhifadhi mbu waenezao ugonjwa wa malaria ambao wanapenda kukaa katika mazingira yasiyosafishwa.
Hayo ameyasema mratibu wa Malaria Mkoa wa Singida Dokta Abdallah Bala alipokuwa anaongea na Standard Radio leo asubuhi.
Dokta Balaa amesema ni muhimu kwa kila mmoja kuwa makini katika kipindi hiki chamvua za masika kinachoendelea mbu huwa wanazaliana sana na kisababisha ugonjwa wa malaria kuongezeka.
Katika hatua nyingine amewaomba watu watumie neti kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria hivyo wanapopewa vyandarua wasivitumie vibaya.
Aidha katika mkakati wa kuzuia mbu Dokta Bala amesema kuwa upo mkakati wa kunyunyizia dawa maeneo mbalimbali ili kuua kabisa mbu.
Ametumia nafasi hiyo kusema kuwa ikifika muda wa jioni kila mtu anapaswa kuvaa nguo ndegu zinazofunika mwili ili mbu wasiweze kukudhuru.
Mwisho.

Post a Comment