Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA
MWENYEKITI wa Mamalishe Tanzania, Havijawa Omary,amewapigia magoti viongozi wa wajasiriamali wa Mkoa wa Singida kuwaomba wamsemee vizuri mama Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili aweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza jana kwenye kongamano la wafanyabiashara wadogo Mkoa wa Singida lililofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwashirikisha machinga,bodaboda,mama na baba lishe,wavuvi,wasusi na mafunzi ujenzi, alisema rais Dk.Samia amefanya mambo makubwa na mazuri kwa wajasiriamali hivyo ni muhimu sana kumuunga mkono.
“Napiga magopi hapa nyie wote hapa ni viongoni ninawaomba mkamsemee mama Samia mazuri aweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huu, Rais amefanya vitu vingi sana na vikubwa sana ndio maana tupo kila mkoa na kushiriki kwenye makongamano kuhakikisha tunayasema yale mazuri aliyoyafanya rais hasa kwenye kundi letu sisi wajasiriamali bila kusahau kundi muhimu la mama lishe,” alisema.
Omary amesema mamalishe na wajasiriamali wengine wamekuwa wanufaika wakubwa katika mikopo inayotolewa na serikali kupitia Benki ya NMB na ile ya asilimia 10 inayotolewa katika Halmashauri za Wilaya kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
“Hatuwezi kuwahamasisha mama lishe watumie nishati safi bila kuona mafanikio, mamalishe ni wanufaika wa kwanza kwenye mikopo aliyoitoa rais, ni kweli mikopo inatoka na mimi nikiwa kama Mwenyekiti wa mamalishe taifa ni mnufaika wa mikopo ya mama lishe inayotolewa na rais kupitia Benki ya Maendeleo ya Jamii,” alisema.
Alisema hivi sasa rais Dk.Samia alishaahidi kuwatengea wajasiriamali shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kutukopesha wafanyabiashara wadogowadogo lengo ni tuweze kuboresha biashara zetu na hivyo kujikwamua na umaskini.
Omary alisema huko nyuma mamalishe walikuwa hawakopesheki kutokana na mazingira ya biashara zao lakini baada ya rais Dk.Samia kuingia madarakani wanapata mikopo kuanzia Sh.100,000 hadi milioni 4.
“Tulikuwa tunanyimwa mikopo sisi mamalishe lakini hivi sasa mambo yetu ni mazuri, kwanini tusisimame kusema mambo mazuri yaliyofanywa na Rais hususani aliyotufanyia sisi mamalishe,” alisema.
Omary aliwasihi wajasiliamali wadogo wadogo kujitokeza kwa wingi kupata vitambulisho vya ujasiriamali ili waweze kupata mikopo inayotolewa katika Benki ya NMB.
“Mama lishe wamekuwa wakilalamika sana lakini kupitia mheshimiwa rais sasa mama lishe tupo ‘smati’ kwasababu tunapata mikopo Benki ya NMB, leo tunatamba sisi hohehae tunapanda mabasi na ndege yote hayo ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, hivi sasa wajasiriamali wote tunaongea lugha moja,” alisema.
Aidha, Omary aliishukuru Idara ya Maendeleo ya jamii chini ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dk.Dorothy Gwajima kwa kazi nzuri anayoifanya ambapo wajasiriamali wamekuwa na heshima hapa nchini.
MWISHO

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Post a Comment