KIJIJI CHA NYUKI KIMETOA MAFUNZO YA KITAFITI NANENANE

 


Na Amini Nyaungo



Waliofika katika Banda la Singida kwenye maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma ambapo Kijiji cha Nyuki walikita kambi wamejifunza taarifa mbalimbali za kitafiti hususani safari za nyuki za namna ya kutafuta maji zinavyofanana na zile za kwenda kutafuta chakula.


Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kijiji cha Nyuki Philimon Kiemi alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma katika hitimisho la Sikukuu za Nanenane Mkoani Dodoma kwa namna nyuki wanavyotafuta maji ndio hivyo hivyo wanavyoenda kutafuta chakula.

Aidha katika maelezo yake amesema kuwa wao wameamua kuja na mzinga wa Nyuki wa  kibiashara ambao ulikuwa kivutio katika maenesho hayo.


" Tumekuja na mzinga wa kibiashara kwa wale waliokuwa wanajifunza kutumia rasilimali za nyuki, tumewafundisha namna safari za nyuki za kwenda kutafuta maji sawa na zile za kutafuta chakula,"Kiemi

Amesema kuwa Mzinga huo unauwezo wa kuvuna mazao mbalimbali kama vile, Gundi la Nyuki, Sumu ya Nyuki, Mkate na Vumbi la Singida.

"Hapa huu Mzinga umekuwa na faida kubwa sana maana linatoa mazao mengi ya kibiashara," Ameongeza.



Aidha hakuacha kusema namna mkoa wa Singida utakavyokuwa kitovu cha utalii kupitia kijiji cha Nyuki.

"Singida itakuwa ni sehemu ya vivutio vya utaliii ambapo watu watakuja kuangalia na kupitia kijiji cha nyuki tutawaleta namna tutakavyoongeza uzalishaji,"Amesema.

Ametumia nafadi hiyo kuipongeza serikali katika sekta ya uvuvi kwa kuwa na droni ambazo zitaweza kuangalia hali ya usalama kwa wavuvi huku akisema kuwa teknolonia hiyo inamfaa yeye kwakuwa kijiji cha nyuki kina wanafunzi kama ataitumia tasnia hiyo basi itakuwa rahisi kuona namna wanafunzi wanavyofika katika mizinga na kuifungua huku akiweka na muda wa kufungua na kufunga.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post