DKT. MGANGA AWAASA WAFANYAKAZI WA UMMA KUACHA RUSHWA

 

Na Amini Nyaungo



Watumishi wa umma wametakiwa kuwa na weledi na uaminifu sehemu wanapofanyia kazi ili tija ya kuwahudumia na kujihudumia ipatikane katika sura ya haki pamoja na utaratibu ili vitendo vya rushwa visipatikane sehemu za kazi.



Hayo ameyasema leo Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida DKT. Fatma Mganga katika semina iliofanyika katika ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ambapo mafunzo yametolewa na Ofisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru.

Dkt. Mganga ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Rushwa sio kutoa hela pekee bali hata utendaji wako wa kazi ikiwa imepangiwa ufanyekazi saa 9 wewe umefanya saa 6 ni sehemu ya rushwa.



“Rushwa sio kutoa pesa pekee bali rushwa ni kufanyakazi au unapofanyakazi kwa maslahi binafsi au unapopunguza saa za kufanyakazi ni sehemu ya rushwa maana utalipwa mshahara uliokamili ambao haujaufanyiakazi,” DKT. Mganga

Aidha amesema kuwa vitendo vyote vilivyo kinyume na maadili na haki za binadamu huwa vina viashiria na rushwa.



Katika semina hiyo ofisa kutoka TAKUKURU mkoa wa Singida Onesmo Mdegela ametoa darsa juu ya hatari ya  kupokea rushwa na makossa yake kwa aliyeomba na kupokea rushwa, amelezea rushwa ya ngono kazini.



Aidha kwa upande wake amesema kuwa rushwa ni adui wa haki kwani inamnyima mtu kupata haki yake ya msingi kwa kuminywa na anayechukua kwa kuwa yupo katika nafasi fulani.

 

Mwisho 


Post a Comment

Previous Post Next Post